Sunday, 27 July 2014

BEI YA BIDHAA YAPANDA KUTOKANA NA MATAYARISHO YA IDDUL-AL-FITR

Kilicho na mwanzo hakikosi mwisho hatimaye waumini wa dini ya kislamu wamefika kIlele cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Waislamu kutoka kila pembe wameanza matayarisho ya sikukuu ya idul fitri ambayo itaadhimishwa jumanne wiki ijaya  na kama ilivyobayana hapa mombasa bei ya bidhaa sokoni imepanda maradufu ishara tosha kuwa waislamu wanajiandaa vilivyo kuhakikisha kuwa siku hiyo wameisherehekea vizuri.
katika pita pita zako utashuhudia vizuri hali ilivyo sokoni na vile watu wamemiminika vizuri kupata chao kizuri angalau waseme kuwa wamepata lao.

No comments:

Post a Comment